KIPI KIASHIRIA CHA MAENDELEO ENDELEVU?A Poem by Peter MmbagaWith 17 Sustainable Development Goals as the roadmap to improves sustainable future for all but achieving all can be determined on what we do now....Uongozi-kichaka cha haja, Hoja ya makini ni lahaja, Ipi tamu kwa waja, Kimvita au Kiunguja, Kwa maendeleo endelevu, Je, ni kiashiria?
Weledi hutengeneza utimilifu, Uongozi bila kujua ‘madhaifu’, Hujenga mashirikiano hafifu, Uzalendo kwa upande-sarafu, Kwa maendeleo endelevu, Je, ni kiashiria?
Elimu na soko la ajira, Au kichaka pora fikra? Elimu ya kusaidia jamii, Imekuwa bidhaa-adui, Kwa maendeleo endelevu, Je, ni kiashiria?
Miti 'deile' inapotea, 'Ozoni leya' inateketea, Uoto asilia unajikaukia, Tegemeo letu ni mkaa, Kwa maendeleo endelevu, Je, ni kiashiria?
Kukua kwa matabaka, Kuishi kwa mashaka, Leo huyu, kesho nani? Kapotea, 'alipo' hajulikani, Kwa maendeleo endelevu, Je, ni kiashiria?
Usawa wa kijinsia-sare? Mimba hupoteza elimu bure, Taifa linaandaa vichwa bure, Au tucheze ngoma 'chao kiherehere' Kwa maendeleo endelevu, Je, ni kiashiria?
‘Yule’ awazuia hawa, Wake wakitamba sawa, Demokrasia bila usawa, Demoghasia kwa wazawa, Kwa maendeleo endelevu, Je, ni kiashiria?
© 2019 Peter Mmbaga |
Stats
30 Views
Added on September 22, 2019 Last Updated on September 22, 2019 AuthorPeter MmbagaDar es Salaam, Dar es Salaam, TanzaniaAboutI'm passionate about writing, when you say a word 'writing' it means your talking about my life story as I can do some kinda writing such like PR writing, author, articles writer, lyrics and poetry e.. more..Writing
|